Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk.Jakaya Kikwete kufungua kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk.Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa mkutano wa Kamati hiyo, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Picha na Bashir Nkoromo.
No comments:
Post a Comment