Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU)
katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa
Mei 25, 2013.
|
RaisDk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa
Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo
jijini Addis Ababa - Mei 25, 2013.
|
RaisDk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa
Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo
jijini Addis Ababa - Mei 25, 2013.
|
Viongozi mbali mbali wa nchi za Umoja wa Afrika (AU)
wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.
|
Marais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50
ya AU katika makao makuu ya
umoja huo jijini Addis Ababa - Mei 25, 2013.PICHA
NA IKULU.
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku tayari kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za
Afrika katika sherehe za miaka 50 tangu
kuanzishwa kwa Umoja wa nchi za Afrika (AU) zilizofanyika katika
makao makuu ya umoja huo.
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa |
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la Afrika waliohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi Jumamosi Mei 25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Shamrashamra
zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati viongozi wa nchi za Afrika
wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole.
Muungano wa Afrika
wakati huo ukijulikana kama OAU, ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis
Ababa, ukianza na nchi za 32 na baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi
kwenda, huku Afrika ya kusini ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994.
Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika
Lusaka, Zambia.
Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka
hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika.
Kauli mbiu ya sherehe
za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na
kuimarishwa kwa muungano huo.
Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini
Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili
na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka 50 ijayo
No comments:
Post a Comment