Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh Josephine Matiro akimuongoza
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,mapema jana alipokuwa akikagua
uhai wa mashina ya chama hicho katika kijiji cha Tandala,Wilaya ya Makete
mkoani Njombe.Kinana na ujumbe wake wako ziarani mkoani Njombe katika
kuimarisha shughuli za chama,kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM
na pia kuzungumza na Wananchi kuhusiana na matatizo yao mbalimbali
yanayowakabili .
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wananchi wa kata ya
Iniho jana ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe,Kinana alizungumza kwenye
mkutano huo wa hadhara mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahakikishia wananchi kuwa
Serikali itaendelea kutekekeleza miradi yake yote iliyoahidi ikiwemo ya
barabara,maji na umeme,aidha aliwataka wananchi kubeza baadhi ya vyama vya
siasa vinanvyoeneza chuki kwa watanzania na kuindosha amani iliyopo.Kinana
akiwa sambamba na ujumbe wake ameyazungumza hayo wilayani Makete katika kijiji
cha Ukwama ikiwa siku ya nne ya ziara yake mkoani Njombe kutembelea mashina ya
chama hicho pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kueleza serikali
ilichotekeleza.
Katibu wa Itikadi na
Uenezi Taifa Nape Nnauye akimtambulisha aliyekuwa mwanachama wa
CHADEMA,Keffa Lupiana pichani kushoto kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo
kwenye kata ya Iniho,Wilaya ya Makete
mkoani Njombe.
Mbunge wa Jimbo la Makete na Naibu Waziri wa Maji
Dkt.Binilith Mahenge akieleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanywa
jimboni mwake katika kutekeleza Ilani ya
CCM kwenye mkutano wa .
Sehemu ya Wananchi
wakishangilia jambo wakati ndugu Kinana alipokuwa akizunngumza nao kwenye
mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa shule ya msingi ya ukwama mapema leo jioni
ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe .
Sehemu ya Wananchi
wakiwa kwenye uwanja wa kata ya Ukwama wakimsubiri Ndugu Kinana azungumze nao mapema leo jioni ndani ya
wilaya ya Makete mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment