Thursday, May 23, 2013

Waathirika wa mafuriko Arumeru Magharibi wapata msaada


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 200 kutoka kwa Meneja  Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani Wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akimshukuru Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (kulia) akizungumza baada ya kupokea msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Twiga Cement kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni. Kulia kwake ni Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (aliyeshika kamba kulia) akisaidia maandalizi ya ujenzi wa daraja sehemu iliyoharibiwa na mafuriko katika hafla ambayo kampuni ya Twiga Cement ilikabodhi msaada wa saruji kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani Wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger