CCM YAVUNA WANACHAMA KIBAO MKOANI NJOMBE - WANACHAMA 160
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa katika picha a pamoja na baadhi ya washiriki walikuwa wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama
Katibu Mkuu wa chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Mji wa Makambako mapema leo jioni wakati alipohitimisha ziara yake ya siku saba mkoani Njombe.Katika hitimisho hilo Ndugu Kinana ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo katika kuimarisha chama,aidha ziara hiyo ilikwenda sambamba na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho cha CCM.Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Polisi mjini Makambako.Katika mkutano huo Kinana alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wapatao 160 walioujiunga na chama hicho.
Katibu Mkuu wa chama cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya chama hicho katika tawi la Mizani mapme leo jioni.
Katibu wa NEC,Itikadi na Unezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mji wa Makambako mapema leo jioni wakati wa hitimisho la ziara ya CCM mkoani Njombe,ikiwa ni siku ya siku saba.
Katibu wa NEC,Itikadi na Unezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Mji wa Makambako mapema leo jioni wakati wa hitimisho la ziara ya CCM mkoani Njombe,ikiwa ni siku ya siku saba.
Wadau wakifuatilia mkutano huo.
Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa kikundi cha Wajasiliamali kutoka kata ya Mjimwema
Baadhi ya Wakazi wa Makambabo wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa polisi,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment