Friday, July 26, 2013

HALMASHAURI ZA MIJI,MANISPAA NA MAJIJI ZATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE MIRADI YA MAJI

Naibu waziri wa Maji Dk Binilith Mahenge azungumza na watendaji wa maji pamoja na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya mjini Moshi.


Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami akichangia jambo katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge(aliyesimama) akizungumza na watendaji wa maji pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi.waliokaa kutoka shoto ni Suleiman Mombo(RSO),Mkuu wa wilaya ya Moshi Dk Ibrahim Msengi na wa mwisho kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA) Cyprian Luhemeja akichangia jambo katika kikao cha naibu waziri wa maji Dk Mahenge na watendaji wa idara ya maji.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

Mhandisi wa maji wilaya ya Moshi vijijini Brown Lyimo akitoa maelezo mbele ya naibu waziri wa maji Dk Mahenge alipotembelea mradi wa maji wa Mbokomu wilaya ya Moshi vijiji
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

Miongoni mwa mambo ambayo yalionekana kumkera Naibu Waziri ni pamoja na upotevu huu wa maji kama inavyoonekana hapa huku wahusika wakiweka mti ili kuzuia maji yasitoke badala ya koki.Hapa Naibu Waziri akimuuliza Mhandisi wa Wilaya kuhusu tatizo hilo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi

SERIKALI imetaka mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini sanjari na halmashauri za miji,manispaa na majiji kuipa kipaumbele miradi ya maji katika maeneo ili kupunguza uwezekano wa kuwapo kwa maradhi ya milipuko yanayochangiwa na ukosefu wa maji safi na salama.

Naibu Waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa wilaya ya Moshi wakiwamo wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa ya Moshi na Moshi vijijini wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kilimanjaro kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.

Amesema kuna umuhimu kwa mamlaka na miji hiyo kutenga sehemu ya fedha katika bajeti zao kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji huku wizara ikiendelea kutoa misaada katika miradi mikubwa na masuala ya kiufundi.

“Lazima mtenge fedha za miradi ya maji kila mwaka,msipofanya hivyo, sisi tunajua hilo siyo jambo la kipaumbele, lakini kumbukeni upatikanaji wa maji unawasaidia wananchi kupunguza fedha ambazo wangetumia kwa matibabu baada ya kuugua matumbo na watazifanyia shughuli za kiuchumi”alisema.

Kuhusu wingi wa maji Naibu Waziri alipongeza juhudi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) kwa kuvitunza vyanzo vya maji Nsere, uchimbaji kisima cha eneo la Longuo, tanki la kuhifadhi maji Kilimanjaro na CCP ambavyo kuna miti yenye kuhifadhi maji.

Akizungumzia mradi wa vijiji 10 unaofadhiliwa na benki ya dunia, alitaka kila halmashauri kuhakikisha unatekelezeka kwa wakati ili kupunguza idadi ya watu wanaokosa maji.

Hata hivyo alikiri kuwapo kwa changamoto ya mgawo wa vijiji 10 hata kwa halmashauri ambazo ni kubwa zenye vijiji zaidi ya 100 ambazo nazo zinatakiwa kuainisha vijiji 10 jambo ambalo alidai linatakiwa kutazamwa upya.

“Lazima tuangalie upya vigezo vya ugawaji wa mafungu ya fedha kwa kuzingatia ukubwa wa Wilaya kwani sasa inazingatia idadi ya watu,aina ya teknolojia ya mradi wa maji,maeneo mengine teknolojia mtiririko ambayo ni gharama sana na mengine ni ya visima au mabwawa”alisema.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger