Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Sophia Simba aliesimama) ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, ameshangazwa na kitendo cha Diwani wa Kata ya Nyandira kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Luanda Zengwe, kushindwa kuwaondolea wananchi wake kero mbalimbali tangu achaguliwe ikiwemo kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Mvomero kuwezesha kupatikana kwa kitanda maalumu cha kubebea wagonjwa.
Badala yake amekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha vijana na wanachama wa chama hicho na pia kuzomea na kuletea fujo viongozi wa serekali ya Chama Tawala (CCM) wanaotembelea kwenye Kata hiyo kwa madhumuni ya kukutana na wananchi ili kupata kero zao mbalimbali na kuzitolea majawabu ya msingi.
Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, alishangwazwa na hatua ya kushindwa kutatua kero hizo na badala yake kuondoka eneo la meza kuu Chadema na kwenda kuwahamasisha wafuasi wake wafanye fujo wakati wa mkutano ulioandaliwa na UWT kwa wananchi wa Kata ya Nyandira.
Diwani Luanda alipandwa na munkari,baada ya Diwani wa zamani wa CCM wa Kata hiyo,Modesta Lubasije kuwasilisha kero kwa Mwenyekiti wa taifa wa UWT juu ya ukosefu wa kitanda cha kubeba wagonjwa "strecha" hasa akina mama wajawazito kwenye Kiji cah Nyandira hali iliyosababisha kutumia machela za miti.
Kutokana na hoja hiyo, Mwenyekiti wa UWT Taifa na Waziri alimgeukia Diwani aliyekuwa ameketi pembezoni mwa meza kuu na kumtaka wakati ukifika atoe ufafafanuzi juu ya kero za Wananchi na wapiga Kura wake,huku akimsisitizia kuwa suala hilo si la Waziri bali lipo chini ya uwezo wa Diwani kwa kushirikiana na Diwani wa Viti Maalumu wa Tarafa ya Mgenta pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya mvomero.
Hata hivyo kufuatilia kuelezwa suala hilo, Diwani huyo alinyanyuka ghafla kutoka meza kuu na kuanza kutoa maneno maneno makali ya kejeli na kumshutumu Waziri Simba kwa kudai swali lililenga kumchafua na hivyo kusababisha kuzuka kwa tafrani za dakika kadhaa na baadaye Mkutano kuendelea kama kawaida.
Kutokana na kitendo chake cha kutoa lugha chafu mbele ya Waziri Simba,aliamua kunyanyuka na kuondoka meza kuu, na kwenda kwa wafuasi wake ambao walijipanga kufanya fujo na kuanza kupiga mayowe na kurushiana vijembe hali iliyowafanya baadhi ya viongozi wa CCM na UWT chini ya Katibu wa CCM Wilaya ya Mvomero,Sadakati Kimati kwenda kumdhibiti Diwani huyo wakisaidiwa na askari Polisi wa eneo hilo.
Waziri Simba aliendelea na Mkutano huo,aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kuchagua viongozi wenye busara na hekima, kwani kitendo cha utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na Diwani wa Kata hiyo ni kuonesha ni namna gani siasa ya vyama vya upinzania zilivyo.
Zengwe ilianza hapa ambapo Diwani wa Kata ya nyandira kupitia Chama cha
dsia na Maendeleo (CHADEMA).Luanda Zengwe (katikati) aliponyanyuka na
kuanza kujibizana na Diwani wa zamani wa CCM wa Kata hiyo, Modesta
Lubasije aliyekuwa akiwasilisha kero mbalimbali kwa
Mwenyekiti wa Taifa
wa UWT, Mhe. Sophia Simba (kushoto).
Katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mvomero,Sadahati kati
akimdhibiti vilivyo Diwani wa kata ya Nyandira kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Luanda Zengwe (mwenye skafu),mbele ya
Askari polisi Sajini t ji, aliyefahamika
kwa jina S.E.Mndeme kutoka kituo cha Polisi mgeta, mara baada ya kutoa
maneno ya lugha chafu kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa (hayupo
pichani) alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata hiyo,Januari 19,mwaka
hu,Diwani lnda alikaribishwa akiwa ni mwakilishi wa wananchi na kuketi
meza kuu.
Diwani wa Kata ya Nyandira kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Luanda Zengwe akiingilia mkutano huo na kuanza kuongea na Wananchi wa Kata hiyo.
No comments:
Post a Comment