Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari Saba waliofariki huko Darfur yawasili nchin

Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini leo majira ya alasili kwa kutumia ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.


Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari wa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni huki Darfur nchini Sudani wakati wakilinda amani,yakishushwa kwenye Ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,Jijini Dar es Salaam Julai 20,2013 alasiri.
Photo by Michuzi

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki duni Darfur wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam Julai 20,2013 alasiri.
Photo by Michuzi

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia huko Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam Julai 20,2013 alasiri.
Photo by Michuzi


Miili ya Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki Dunia wakati wakiwa katika kazi ya kulinda amani kwenye Mji wa Darfur nchini Sudan,imewasili nchini leo majira ya alasili kwa kutumia ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa

Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.

Jeshi la JWTZ lilitoa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni pigo kubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger