Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC
kwa kuendelea na semina, leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na
Kutoka
kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza jana,
na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk.
Sheni na Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya
kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia
Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya
kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape
na
Zakia Meghji na juu-kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akisalimia wajumbe.
Na Kulia chini ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhamed Seif
Khatib na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Vuai Ali Vuai wakiteta jambo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai
Ali Vuai kabla ya kikao kuanza
Wajumbe wa NEC Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika
wakibadilishana mawazo ukumbini
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Dk. Asha-Rose Migiro akichati jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kikao
Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo
hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni
Mjumbe wa NEC, William Mukama akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC
Profesa Juma Kapuya ukumbini
Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na
kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo
HII UNAONAJE?
Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na
Mzee Mtandika
Katibu Mkuu wa UWT, Sophia Simba akijadiliana
jambo wa Wajumbe wenzake wa NEC ukumbini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo
Ana Makilagi.
Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na
Nape
TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO?
Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika
mazungumzo yao
ukumbi kabla ya kikao
HAPO VIPI? Katibu wa Oganaizesheni Dk.
Muhammed Seif Khatib anaonekana kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,
Vuai Ali Vuai wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kikao kuanza
SALAMU! Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa,
Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC ukumbini kabla ya
kikao kuanza
Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza
Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal
(kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe
kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu
kabla ya kikao kuanza
Aliyekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha
Abdallah Juma aka Mama Mshua (kulia) akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani
Madabiba nje ya ukumbi. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba
ENZI ZETU ZA IGUNGA VIPI? Naibu Katibu Mkuu
wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba anaonekana kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge wa
Igunga Dk. Dalaly Kafumu walipokutana
nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza
SHIKAMOO BOSI WANGU WA ZAMANI! Kaim Katibu wa
CCM wa mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda akiwa na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, William
Mukama nje ya Ukumbi. Sixtus amewahi kuwa Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi
na Uenezi kabla ya kuhamishiwa Morogoro mwaka jana wakati Mukama akiwa Katibu
Mkuu wa CCM Taifa.
CCM MAMBO SAFI TU! Mukama akimwambia Mjumbe wa NEC,
Steven Wasira nje ya ukumbi
Wajumbe wa NEC wakiangua kicheko cha
kutaniana kaba la kuingia ukumbini. Kutoka kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari
Makamba, Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta
Wajumbe wakiwa tayari kuingia ukumbini kuanza
kikao leo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dk.Shukuru Kawambwa akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa
Gaudencia Kabaka wakati wa Mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ambapo
leo semina juu ya Mikakati ya Kuondoa tatizo la ajira nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Ndugu Mwigulu
Nchemba akijadiliana jambo na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa wakati wa semina juu ya kuondoa
tatizo la ajira nchi.
Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi na Katibu wa
NEC,Uchumi na Fedha wakijadili jambo la ajira kwa nchi nzima wakati wa semina
ya mikakati ya kuondoa tatizo la ajira nchini, leo kwenye ukumbi wa NEC,Dodoma.
Wajumbe wakiwa kwenye semina ya Mikakati ya
Kuondoa tatizo la ajira nchini.
Ally A. Msaki akitoa mada juu ya HALI YA
AJIRA NCHINI NA MIKAKTI YA SERIKALI kwa niaba ya Waziri wa Kazi na Ajira,kwa
wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inayofanyika Dodoma leo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini
semina juu ya Mikakati ya kuondoa tatizo la Ajira Nchini
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment