Monday, February 11, 2013

UCHAGUZI KAMATI KUU YA CCM WAFANYIKA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura, wakati wa uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, jioni hii, wakati wa Kikao cha NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Makatibu wa NEC, Zakia Meghji (Uchumi na Fedha) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) wakipiga kura,  wakati wa uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, jioni hii, wakati wa Kikao cha NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger