Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Utafiti wa Mitambo ya Nyuklia, Kitengo cha Matengenezo, Yesaya Sungita, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa Mashine ya kutafiti Vyakula na Mazingira, Remigius Kawala, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akionyeshwa baadhi ya maeneo ya Taasisi hiyo, wakati alipotembelea katika Taasisi hiyo iliyopo Njiro jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania na kuhudhuriwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh. Gaudensi Lyimo (kushoto wa kwanza walioketi) iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, baada ya kuzungumza nao alipotembelea Taasisi hiyo Juni 25, 2013. Picha na OMR
Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment