Tuesday, July 23, 2013

WANAJESHI WALIOUAWA NCHINI SUDAN WAZIKWA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,aongoza Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Dafur nchini Sudan.


Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya kuwasilim katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni,Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally iliyosomwa katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika kuwaswalia Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally ,mbele katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) na viongozi wengine walihudhuria katika mazishi ya Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa ni miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa hivi karibuni Nchini Sudan Jimbo la Daafur.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa leo,mchana.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Vingozi na Waislamu,wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger