Monday, July 22, 2013

Mbinu za kujua simu feki

Soko la simu kwa sasa linakabiliwa na matatizo mengi yakiwamo ya kuenea kwa simu feki na ndiyo maana wameamua kuwa na mfumo wa E Warranty ili kuwawezesha wateja wao kuepukana tatizo hilo.



Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya Samsung, Sylivester Manyara akiongea na simu na mmoja wa washindi wa mwezi Juni ambao ni wateja walionunua bidhaa za kampuni hiyo hatimaye kuingia kwenye droo. Washindi hao walipewa zawadi malimbali. Mpigapicha wetu
Na Sweetbert Lukonge 

 

Dar es Salaam. 

Kampuni ya SamSung maarufu kwa kuuza simu, imeamua kuwasaidia wateja wake kwa kuwapa mbinu za kutambua simu bandia kabla ya kutoa fedha wakati wa kununua.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo, Sylvester Manyara alisema mbinu hiyo ni kuanzishwa kwa mfumo maalumu unaoitwa E Warranty ambao una uwezo wa kuzisoma simu za kampuni hiyo ambazo siyo bandia.

Manyara alisema mfumo wa E Warranty unawezesha watumiaji wa simu za Samsung kutambua simu feki ambazo zipo sokoni zikiwa na nembo ya kampuni hiyo.
‘’Kampuni ilibuni mfumo huo baada ya kuona zipo kampuni zilizoamua kutengeneza kwa kuigiza simu za .Samsung’’ alisema.

Alisema soka la simu kwa sasa linakabiliwa na matatizo mengi yakiwamo ya kuenea kwa simu feki na ndiyo maana waliamua kuwa na mfumo wa E Warranty ili kuwawezesha wateja wao kuepukana tatizo hilo.

“Ili kujua kama simu ni halali, mtumiaji anatakiwa kuandika kwenye ujumbe neno Check likifuatiwa na alama ya nyota kisha namba ya ya simu iliyomo ndani karimu na herufi za ‘IMEI’ ikifuatiwa na alama ya reli. Baada ya kufanya hivyo ujumbe huo autume kwenda katika namba 15685 na baada ya ya muda atapa majibu yatakayokuwa yakielezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung,” alisema Manyara.

Katika hatua nyingine zaidi ya watumiaji 10 wa simu za Samsung ambao wamejisajili kwenye mfumo huo wa E warant walijipatia zawandi mbalimbali baada ya kuibuka washindi katika bahati nasibu inayoendeshwa na kampuni kwa wateja wake waliojiunga na huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger